Tukio
hilo limetokea leo majira ya asubuhi muda mfupi baada ya Profesa
Tibaijuka kufungua mkutano wa Kimataifa unaohusu upatikanaji wa majisafi
na usafi wa mazingira, mkutano unaoendelea jijini Dar es Salaam ambapo
yeye alikuwa mgeni rasmi.
Profesa
Tibaijuka ni Mwenyekiti Mstaafu wa Baraza la Kimataifa la Ushirikiano
wa Upatikanaji wa Maji Safi na Salaam lijulikanalo kwa kifupi kama WSSCC
ambalo pamoja na mambo mengine ndiyo linalohusika na mfuko wa dunia wa
ufadhili wa miradi ya maji ambao unafadhili miradi kadhaa ya upatikanaji
wa maji katika wilaya kadhaa za mkoa wa Dodoma.
EATV
imefanikiwa kuzungumza na Profesa Tibaijuka ili kufahamu sababu za
kutumia usafiri huo unaoonekana kutumiwa zaidi na watu wa kipato cha
chini na haya yalikuwa majibu yake "Unajua mimi ni mbunge, ukiwa mbunge
ni mwakilishi wa watu kwa hiyo sina tofauti yoyote na wale watu
ninaowawakilisha," amesema Profesa Tibaijuka.
Ameongeza
kuwa " sasa hivi natakiwa kuwahi ndege uwanja wa ndege kwenda mjini
Dodoma kuhudhuria vikao vya bunge vinavyoendelea huko kwa hiyo badala ya
kutumia usafiri wangu ni bora nitumie hii bajaj ambayo kwa kweli ni
msaada sana pale unapotaka kuwahi mahali,"
Idadi
kubwa ya wageni waliohudhuria mkutano huo ambao wengi ni kutoka nje ya
nchi hawakuamini kile kilichokuwa kikitokea kwani ni nadra kwa kiongozi
wa hadhi yake ambaye amewahi kushika nyadhifa kubwa ndani ya Umoja wa
Mataifa na taasisi mbali mbali za kimataifa kutumia usafiri unaoonekana
kama ni wa hadhi ya chini.
"Huyu
kweli ni kiongozi wa watu, mengi yanaweza kusemwa lakini huyu
anaonyesha utu na upendo kwa watu anaowaongoza," alisikika mshiriki
mmoja akisema kwa mshangao na kuongeza kuwa hata miradi ya maji
iliyotekelezwa chini ya uongozi wake,jimboni kwake na hata mkoani Dodoma
inaonyesha dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi.
Awali
katika mkutano huo, Profesa Tibaijuka amesema suala la upatikanaji wa
majisafi na salama ni muhimu iwapo nchi inahitaji kutokomeza umaskini na
kwamba wananchi wanachotakiwa kufanya ni kuzingatia usafi wa mazingira
na miili yao kwa kufuata kanuni za afya bora.
Profesa
Tibaijuka ameongeza kuwa "Wakati wa uhai wake Mwalimu Nyerere aliwahi
kusema kuwa umaskini sio chanzo cha uchafu bali ni tabia ya mtu..hivyo
basi licha ya umaskini tulionao kama taifa sio sababu ya uchafu kutawala
majumbani kwetu na kuwa chanzo cha magonjwa....kuna haja ya jumuiya ya
Kimataifa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na rais Dkt John Pombe
Magufuli za kutokomeza uchafu katika jamii kwani kama kiongozi wa nchi
yeye mwenyewe ameonekana akichukia uchafu kwa vitendo,"
Kwa
upande wake, Mratibu wa Baraza hilo hapa nchini, mhandisi Wilhelmina
Malima amesema Tanzania inahitaji uwekezaji mkubwa kwenye miradi ya maji
safi na salama na hivyo kuiwezesha kutekeleza lengo namba sita kati ya
malengo kumi na saba endelevu ya Umoja wa Mataifa ambayo hujulikana kwa
kiingereza kama Sustainable Development Goals au kwa kifupi SDGs.
0 comments:
Post a Comment