Polisi Mwanza Wapambana na Majambazi kwa Saa 16, Waua watatu
Watu watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi,wameuawa katika majibizano ya
risasi na askari polisi mkoani Mwanza,alfajiri ya kuamkia jana jumapili
katika mapango ya mlima wa Utemini yaliyopo kata ya Mkolani jijini
Mwanza.
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza Ahmed Msangi,amewataja majambazi
waliouwa katika majibizano ya risasi usiku kucha kuwa ni Omar Francis
Kitaleti mkazi wa Nyegezi Kona,said Khamis Mbuli maarufu kama fundi
bomba mkazi wa bugarika na jambazi mwingine ambaye jina lake bado halijafahamika.
0 comments:
Post a Comment