.

.

Wanafunzi kushiriki Utamaduni wa China

Balozi wa China nchini, Dk Lu Youqing.
Balozi wa China Tanzania, Dr. Lu Youqing

WANAFUNZI 10 kutoka shule za sekondari na vyuo vikuu nchini wamechaguliwa kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya kidunia ya Lugha na Utamaduni wa China baadaye mwezi huu katika Jiji la Beijing nchini China.
Mashindano hayo yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma kwa kuandaliwa na taasisi hiyo ijulikanayo kama “Confucious Institute” kutoka makao makuu yake yaliyopo katika mji wa Harban nchini China, wanafunzi hao 10 wataondoka nchini Juni 28 ili kuungana na wenzao wa mataifa mengine kushiriki mashindano hayo.
Akifungua mashindano hayo mwishoni mwa wiki chuoni hapo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Confucius Institute ya Chuo Kikuu cha Dodoma, Amber Zheng alisema mashindano hayo yanayojulikana kama “China Bridge Competition” yanayoandaliwa na taasisi hiyo na washiriki wake ni wanafunzi wanaosoma na kujifunza Kichina shuleni na vyuo vikuu vya nje ya China.
Ni wenye umri zaidi ya miaka 16, hufanyika kila mwaka ili kukuza uelewa wao zaidi katika taaluma hiyo na pia kujenga mahusiano zaidi kati ya Taifa la China na mataifa mengine duniani.
Alieleza utaratibu wa mashindano hayo kwamba kwa mwaka huu yanafanyika Chuo Kikuu cha Dodoma kwa ngazi ya Kitaifa na washiriki waliofaulu kutoka katika shule na vyuo mbalimbali nchini tayari wamefika kushiriki kupata wale 10 bora watakaokwenda Beijing.
Alisema jumla ya washiriki 23 wanatoka vyuo vikuu vya Dodoma, Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro na Chuo Kikuu cha Ushirika cha Moshi. Vingine ni kutoka Chuo cha Elimu ya Biashara tawi la Dodoma, Shule ya Sekondari ya Lord Barden ya Dar es Salaam na Shule ya Sekondari ya Viwandani kutoka Manispaa ya Dodoma.
Upimaji ulijumuisha hatua tatu ambazo ni kuandika, kuongea na usomaji lafudhi au sarufi za Kichina na pia uimbaji na uchezaji nyimbo na mitindo ya tamaduni za China. Waliofaulu ni Kennedy Edward na Tony Thomas kutoka Shule ya Sekondari ya Lord Baden, Abdul Hassani kutoka Shule ya Sekondari ya Viwandani, Hamis Likoko, Faraja Mwapule, Eliabu Mwita na Eliuta Mangula wote kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma. Pia yupo Harrison Miraji kutoka Chuo Kikuu cha Ushirika cha Moshi pamoja na Said Mwanisenga na Abdullah Mwinyiabu wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro.
Share on Google Plus

About UPStream Telecom

0 comments:

Post a Comment