.

.

Huduma za kibenki sasa mpaka mlangoni mwa mteja

 Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Abdi Mohamed
Mkurugenzii mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Abdi Mohamed
BENKI ya Barclays Tanzania imesema ufunguzi wa matawi mapya unaofanyika utaiwezesha kuwa karibu zaidi na wateja kuwasaidia kuwahudumia. “Tunaamini katika kuhudumia vyema wateja wetu katika kila wafanyacho.
Na kwa kufungua matawi haya mapya tutakuwa karibu zaidi kuwasaidia kutambua malengo yao ya kifedha,” alisema Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Biashara, Kumaran Pather. Alisema hayo hivi karibuni kwenye ufunguzi wa tawi lao katika Jengo la Mwanza Rock City Mall, jijini hapa.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Abdi Mohamed, alisema ni faraja kwa benki hiyo kufungua tawi kwenye jiji la Mwanza linalokua kwa kasi. Alisema uzinduzi huo unamaanisha kuwa sasa wanaweza kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya mji wa Mwanza.
Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Mkuu wa Usambazaji wa Barclays Africa Group, Vimal Kumar . Naye Kumar alisema “Nimesafiri kutoka Afrika Kusini kuja Tanzania kukutana na wateja wetu, kuwahakikishia kuhusu dhamira yetu kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla na tukio hili muhimu la uzinduzi wa tawi jipya hapa Mwanza”.
Share on Google Plus

About UPStream Telecom

0 comments:

Post a Comment