.

.

Tyson Fury anafaa kupigwa marufuku, asema Klitschko



Image copyrightAP
Image captionTyson Fury

Bondia wa uzani mzito duniani Tyson Fury anafaa kupigwa marufuku katika mchezo wa ndondi kwa matamshi yake ambayo yanamfananisha na Hitler,Wladimiri Klitschko amesema.
Fury aliomba msamaha mwezi uliopita baada ya kuchapisha kanda ya video mtandaoni ilio na ubaguzi,ujinsia na maneno yanayokashifu Wayahudi.
Lakini bingwa wa zamani katika uzani huo Wladmir Klischko ambaye atakabiliana na Fury mjini Manchester tarehe 9 mwezi Julai ,alisema: nilishangazwa na taarifa yake.


Image copyrightGETTY
Image captionNdondi

Wakati alipokuwa akiongea kuhusu Wayahudi alizungumza kama Hitler.''Mtu huyu ni mpumbavu''.
Raia huyo wa Ukrain ambaye alipoteza kwa Fury mnamo mwezi Novemba na hivyobasi kupoteza kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 11 aliongezea,''hatuwezi kuwa na bingwa kama huyu''.
''Ni lazima anyamazishwe ama anyamazishwe katika ulingo wa ndondi,kwa sababu huwezi kuongeza chuki zaidi''.


Image copyrightAFP
Image captionWladmir Klitschko

''Ninapigana na mtu ambaye hawezi kufunga mdomo kuhusu maswala fulani''.
Share on Google Plus

About UPStream Telecom

0 comments:

Post a Comment